IDARA YA POLISI MJINI MINNEAPOLIS YAVUNJWA KUFUATIA KIFO CHA FLOYD | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 8, 2020

IDARA YA POLISI MJINI MINNEAPOLIS YAVUNJWA KUFUATIA KIFO CHA FLOYD

  Malunde       Monday, June 8, 2020

Idara ya polisi mjini Minneapolis katika jimbo la Minnesota nchini Marekani itafanyiwa mabadiliko makubwa kutokana na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd. 

Halmashauri ya jiji hilo imekubaliana kuivunja kabisa idara ya polisi na kuweka muundo mpya wa utendaji kazi wa polisi. 

Hayo ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa Baraza la mji huo Lisa Bender. 

Floyd aliuawa mikononi mwa polisi chini ya wiki mbili zilizopita mjini humo tukio ambalo lilizusha maandamano ya kitaifa nchini Marekani na mengine mengi katika nchi mbalimbali. 

Mwaka jana, afisa mmoja wa polisi wa zamani mjini Minneapolis alihukumiwa kifungo cha miaka 12 na miezi sita jela kwa kumpiga risasi na kumuuwa mwanamke mweupe wa Australia ambaye hakuwa na silaha yoyote, wakati akitoa habari ya tukio la uhalifu.

-DW


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post