CHINA KUFUTA BAADHI YA MIKOPO KWA MATAIFA YA AFRIKA


China imesema itafuta mikopo isiyokuwa na faida iliyokuwa kama mzigo kwa mataifa mbalimbali ya Afrika wakati huu bara hilo linalopoendelea kukabiliana na janga la Corona.

Rais Xi Jinping ametoa tangazo hilo na kuongeza kuwa mataifa yaliyoatiriwa zaidi na virusi hivyo vitapewa muda wa kulipa madeni wanayodaiwa.

Akizungumza na viongozi wa nchi hizo kupitia mfumo wa Video, rais Jinping pia amezitaka taasisi za fedha za China kuwa na mazungumzo ya kirafiki na nchi za Afrika kuona namna watakavyolipa madeni yao.

Aidha, katika hatua nyingine, amesema nchi yake itasimama na bara la Afrika katika vita dhidi ya Corona na kufadhili ujenzi wa makao makuu ya kudhibiti magonjwa barani Afrika jijini Addis Ababa.

Bara la Afrika kwa sasa lina maambukizi zaidi ya Laki Mbili na vifo zaidi ya Elfu saba kutokana na janga la Corona.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527