CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA HICHO


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kujitokeza kuanzia leo Juni 3 hadi Juni 15 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, amesema taarifa za kusudio la kugombea urais kupitia chama hicho zinapaswa kuwasilishwa katika ofisi ya Katibu Mkuu na baadae zitajadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho na kutolewa uamuzi.

“Kwa mamlaka niliyopewa na kanuni hii ya chama ninaomba kutangaza sasa tarehe za mwanzo wa zoezi hili na tarehe za mwisho wa zoezi hili la kutangaza nia ya kusudio la kugombea milango hii imefunguliwa kuanzia tarehe ya leo mpaka tarehe 15 ya mwezi Juni” amesema Mnyika

Licha ya suala hilo la urais Katibu Mkuu huyo pia amesema kuwa chama hicho kimefungua milango ya ushirikiano na vyama vingine kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu na vyama ambavyo ameviita ni vyama makini.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527