WENYE VIRUSI VYA CORONA NCHINI KENYA WAFIKA 607


Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona, hii ni baada ya watu  632 kupimwa katika muda wa saa 24 zilizopita  na kufanya jumla ya wealioambukizwa kufikia  607.

Wagonjwa hao ni wakenya 22,raia mmoja wa Tanzania,mmoja wa Uganda na mmoja wa China.

Naibu waziri wa afya Dkt Rashid Aman ametoa wito kwa wakazi wa Mtaa wa Eastleigh kufuata kanuni zilizotangazwa na wizara ya afya kusalia nyumbani baada ya idadi kubwa ya watu kudaiwa kuhamia mitaa mingine.

Aidha idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 29 baada ya watu watatu zaidi kufariki.

Idadi ya waliopona imefikia 197 baada ya watu 7 zaidi kupona.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527