WATANZANIA WALIOKWAMA INDIA WAREJEA NCHINI, KUISHUKURU SERIKALI


Ubalozi wa Tanzania nchini India, kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Tanzania [Air Tanzania] pamoja na Diaspora wa Tanzania nchini India wamefanikisha safari ya kwanza ya kuwarejesha nchini watanzania waliokuwa wamekwama katika miji mbalimbali nchini India kutokana na zuio la kuingia na kutoka ndege za Kimataifa lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Ndege maalum ya Boeng 787-8 ya Dreamliner ya Air Tanzania ilitumwa na Serikali Jijini Mumbai kwenda kuwachukua watanzania hao waliokwama nchini India tangu tarehe 22 Machi 2020 lilipowekwa zuio hilo na Serikali ya India.

Ndege hiyo imeondoka India leo tarehe 15 Mei 2020 saa 2 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji International Airport, Mumbai ikiwa imebeba jumla ya raia wa Tanzania 246, miongoni mwao ni waliokuwa wameenda India kwa ajili ya matibabu, wahitimu kutoka vyuo mbalimbali na wanafunzi ambao wanalazimika kurudi nyumbani kwa kuwa vyuo vimefungwa hadi mwezi Agosti/Septemba 2020.

Ndege hiyo imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere [JNIA] mnamo saa 6 mchana leo Ijumaa tarehe 15 Mei 2020.

Takriban watanzania 410 walijiandikisha katika Ubalozi wa Tanzania, New Delhi na kuelezea utayari wao wa kuchangia gharama.

Kwa kuwa idadi ya watanzania waliojitokeza ilikuwa kubwa zaidi ya waliweza kusafiri katika awamu hii ya kwanza, Serikali inaangalia uwezekano wa kutuma ndege nyingine maalum ya Air Tanzania kuja kuwachukua raia waliosalia ndani ya mwezi huu.

Gharama ya tiketi ya ndege hiyo, namna ya kulipa, Mahali ambapo ndege itatua pamoja na tarehe za kuwasili kwa ndege hiyo nchini India zitatangazwa na Ubalozi mapema iwezekanavyo.

Ubalozi unapenda kuwashukuru Diaspora wa Tanzania nchini India kwa kufanikisha zoezi hili kwa weledi mkubwa na Uongozi wa Wizara za Mambo ya Nje za India na Tanzania na Serikali, kwa ujumla, kwa miongozo mbalimbali wakati wa zoezi hili.

Kabla ya ndee hiyo kuwasili katika uwanja wa ndee wa Kimataifa wa Julius Nyerere wazazi, nduu na jamaa wa watanzania hao walionekana wakiwa na nyuso za furaa huku wakiwasubiria ndugu zao.

Mmoja kati ya wanafunzi waliokuwa wanasoma India, Sulemani Khalidi ameishukuru sana Serikali kwa kuwarejesha…. “Kwa kweli naishukuru sana Serikali yangu kwa kusirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kutusaidia sisi sote hadi kufika hapa nchini leo,”. Amesema Khalidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527