WAGONJWA WA CORONA UGANDA WAFIKA 227


Uganda imetangaza visa vipya 24 vya COVID19 vimeongezeka na vyote vikiwa ni vya Madereva wa Malori na kufanya jumla ya visa kufikia 227.


Wizara imesema jumla ya sampuli 2,598 zimepimwa kati ya hizo; 2,044 ni za Madereva wa malori na 554 ni za Wakazi wa Uganda ambapo zote 554 zimeonekana hazina maambukizi

Katika visa hivyo 24, Waganda ni 3 na Wakenya 2 ambao hao wamegundulika katika mpaka wa Elegu. Wengine waliogundulika katika mpaka wa Mutukula ni Watanzania 6 na Mganda mmoja. Pia, Wakenya 12 waliogundulika katika mpaka wa Malaba

Lakini pia, Jumla ya Wagonjwa 63 wamepona nchini humo tangu kuzuka kwa janga hilo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527