WAGONJWA WA CORONA NCHINI UGANDA WAFIKA 139


Taarifa ya Wizara ya afya nchini uganda kwa vyombo vya habari inaashiria maambukizi mapya 13 ya kirusi cha Corona na kuifikisha idadi ya visa kuwa 139.


Wagonjwa wapya wote ni Madereva wa Malori ambapo kati yao Waganda ni 7, Wakenya 5 na Raia wa Eritrea mmoja  aliyepitia Sudan Kusini,Kenya,Tanzania na kisha Uganda kupitia mpaka wa Mtukula.

Takribani sampuli 2,104 zimefanyiwa vipimo,miongoni mwazo 1741 zikiwa za madereva huku 363 kutoka maeneo tofauti ya ndani mwa Uganda.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527