CHADEMA MARA YAMFUTIA UANACHAMA DIWANI MARRY ELIAS NYAGABONA


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MKOA WA MARA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, kupitia kikao chake  cha dharura cha Baraza la Uongozi la Mkoa, kilichoketi leo tarehe 12/05/2020 kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 7.5.2(a) pamoja na mambo mengine kikao kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Mkoa na nidhamu ya Viongozi ndani ya Chama.


Katika kikao hicho, baada ya kujadili kwa kina hali ya mwenendo wa Madiwani wetu ndani ya Mkoa, Baraza la Uongozi la Mkoa wa Mara limeazimia kumfutia uachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mhe. MARRY ELIAS NYAGABONA ambaye ni Diwani wa Viti Maalum (CHADEMA).

Hii ni kutokana na kuthibitika wazi kuwa MARRY ELIAS NYAGABONA amekuwa akipingana na Itikadi, Sera, na Falsafa ya CHADEMA hivyo kumfanya kupoteza sifa za kuwa mwanachama wa CHADEMA kwa mujibu wa Ibara ya 5.1.4 na 5.1.5 ya katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 Toleo la Mwaka 2019.

Kwa taarifa hii, MARRY ELIAS NYAGABONA kwa kufutwa kwake uanachama, anapoteza udhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hivyo kupoteza sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa Viti Maalum.

LUCAS NGOTO
MWENYEKITI WA CHADEMA
MKOA WA MARA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527