TRUMP AAMURU NYUMBA ZA IBADA ZIFUNGULIWE ILI WATU WAENDELEE KUSALI NA KUOMBA KWA AJILI YA CORONA


Rais  wa Marekani  Donald Trump amewaagiza Magavana wa Majimbo Nchini humo kufungua  nyumba zote za ibada  na Ibada ziendelee huku akisisitiza Watu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona. 


Trump amesema nyumba za ibada ambazo  ni pamoja na makanisa, masinagogi na misikiti ni maeneo yanayotoa huduma muhimu kwa jamii. 

Aidha amesema ikiwa magavana hao hawatotimiza agizo lake, basi atachukua hatua mikononi mwake kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo 

“Nyumba za Ibada  zinawaleta Watu pamoja na kuwaunganisha, fungueni, mwenye swali anipigie ila hatofanikiwa"- Alisema Trump

Maagizo ya Trump yametafsriwa na wengi kama hali flani  ya kukubaliana na Msimamo wa Rais wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikataa kuwafungia watu ndani kisa Corona na akasisitiza watu Wamuombe Mungu huku wakiendelea kuchukua tahadhari .


Dr Magufuli amekuwa akikaririwa mara kadhaa akisema kuwafungia watu kunawapunguzia kinga zao na hata kupuliza dawa barabarani hakuondoi Virusi vya Corona  na kwamba  Corona ni ugonjwa ambao utachukua muda mrefu kuisha kama ilivyo UKIMWI na magonjwa mengine.



Msimamo huo wa Rais Magufuli uliungwa mkono na Shirika la Afya Duniani WHO ambalo hivi karibuni lilitoa waraka ukisema kupuliza Dawa barabarani au sehemu za wazi hakuondoi virusi vya Corona, kujifungia ndani kunapunguza Kinga na kwamba ugonjwa huu utachukua muda mrefu kuisha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527