TBS YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUTUMIA VIPIMO SAHIHI KUPATA BIDHAA ZILIZO BORA


Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Athuman Ngenya (Katikati) akizungumza na wanahabari katika ofisi za TBS jijini Dar es Salaam leo.

******
NA EMMANUEL MBATILO 
Shirika la viwango Tanzania (TBS) kushirikiana na taasisi nyingine zenye dhamana ya kushughulika na vipimo wamejipanga kuhakikisha kila mfanyabiashara anayezalisha bidhaa yake hapa nchini atumie vipimo sahihi ili kupata bidhaa zenye ubora kwa matumizi ya Watanzania na nje ya nchi.

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Athuman Ngenya katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambayo hufanyika Mei 20 kila mwaka.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi za shirika hilo Jijini Dar es Salaam Dkt.Ngenya amesema kuwa Serikali imejielekeza kwenye kuhakikisha kunakuwa na viwanda vya kutosha ili kuweza kutoa ajira za kutosha, kufanya biashara kukuza uchumi wa binafsi na maendeleo ya nchi kwa ujumla ila ni vyema pia tukazalisha bidhaa zenye ubora.

"Nataka niwaambie wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara kuwa Tanzania kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango inawezekana, TBS kupitia maabara yake ya ugezi (Metrology Laboratory ndio watunzaji wa viwango vya kitaifa vya vipimo. Kwa sasa maabara ya ugezi inauwezo wa kutoa huduma za mafunzo ya sayansi ya vipimio na upimaji katika maeneo ya uzito/Tungamo,Urefu,Hali joto,Ujazo mdogo na Mkubwa,Mgandamizo,Kani,Umeme,Toku na Kemikali". Amesema Dkt.Ngenya.

Aidha Dkt.Ngenya amesema kuwa kila mwaka siku ya vipimo dunaiani imekuwa ikiadhimishwa kauli mbiu tofauti na mwaka huu wanasayansi wa vipimo duniani kote wanasherekea siku hii ya vipimo kwa kauli mbiu inayosema Vipimo kwa Biashara Duniani..

"Biashara Kimataifa inaweza kufanyika kwa urahisi iwapo uzalishaji katika viwanda vyetu utafanyika kwa kuzingatia vipimo sahihi vilivyopo kwenye kila kiwango cha bidhaa husika". Amesisitiza Dkt.Ngenya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post