JKCI YAKANUSHA KUHUSIKA NA MASHINDANO YA MBIO ZA HEART MARATHON 2020


Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuujulisha Umma kuwa haihusiki kwa njia moja au nyingine na mashindano ya mbio za Heart Marathon 2020 yaliyokuwa yafanyike  tarehe 19 Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam na Zanzibar na kuahirishwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID – 19).


Mbio hizo za Heart Marathon ambazo zimepangwa kufanyika siku za mbeleni zimeandaliwa  na Asasi ya kiraia ya Tanzania Health Summit na siyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Aidha Taasisi inatoa rai kwa wananchi watakaopenda kushiriki katika mashindano hayo kuwasiliana moja kwa moja na waandaaji  kama matangazo yao yanavyoonesha.

Hata hivyo kama unapenda kuchangia sehemu ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika Taasisi yetu unakaribishwa. Unaweza kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia  namba ya malipo ya Serikali 994830000022.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527