AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI KISA MZIGO WA DENI LA MKOPO BENKI

Na Esther Macha, Mbeya
Mfanyabiashara mkazi wa Mtaa wa Ibala Kata ya Uyole Jijini Mbeya, Jonas Mahenge (52) amejiua kwa kujipa risasi mdomoni na kutokea utosini baada ya kukwama kufanya marejesha ya mkopo anaodaiwa na Benki ya CRDB.

Akizungumzia tukio hilo leo, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya,Ulrich Matei, alisema tukio hilo limetokea Mei 18, 2020 saa 3.00 usiku katika Mtaa wa Ibala Kata ya Uyole.

Amesema mfanyabiashara huyo alijiua kwa kutumia bastola aina ya Pisto Browning yenye namba A920533 Car namba za usajili 00099307.

Kamanda Matei amesema, hivi karibuni marehemu aliomba mkopo katika Benki ya CRDB kiasi cha sh. milioni 100, lakini baadaye marejesho ya fedha hizo yalianza kumtatiza akaamua kuuza nyumba yake kwa ajili ya kupunguza deni hilo.

Baadaye benki ilimpa sharti la kuwa anarejeshe kila mwezi sh. milioni 3, kitu ambacho alishindwa kutokana na biashara ya madini alizokuwa akizifanya Chunya alikowekeza fedha kutokuwa anapata faida.

Mei 18, 2020 wanafamilia waliamka usiku saa nane kwa ajili ya kujifukiza kwa ajili ya magonjwa mbalimbali.

 Alisema wakati wenzake wameamka na kwenda kwenye maandalizi ya kujifukuzia dawa, yeye (sasa marehemu) alirudi na kujifungia ndani akachukua silaha yake na kujipiga risasi mdomoni ikatokea kisogoni/utosini.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527