Picha : SHIRIKA LA RAFIKI SDO LATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KWA WAWEZESHAJI WA VIKUNDI VYA MABINTI BALEHE SHINYANGA


Sehemu ya ndoo na sabuni zilizotolewa na Shirika la Rafiki SDO kwa Wawezeshaji wa Vikundi vya Mabinti ngazi ya kata katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka shirika la Rafiki SDO, Dkt. Juma Jilala (kushoto) akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID-19 Mwezeshaji Vikundi vya Mabinti kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Queen George.
Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka shirika la Rafiki SDO, Dkt. Juma Jilala (kushoto) akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID-19 Mwezeshaji Vikundi vya Mabinti kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Anna Mkina.
Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka shirika la Rafiki SDO, Dkt. Juma Jilala (kushoto) akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID-19 Mwezeshaji Vikundi vya Mabinti kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Grace Emmanuel.
Afisa Mwezeshaji Uchumi kwa Mabinti ngazi ya wilaya kutoka Shirika la Rafiki SDO, Asante Nselu (kulia) akikabidhi  vitendea kazi kwa Wawezeshaji vikundi vya mabinti. 
Wawezeshaji Vikundi vya Mabinti wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa vifaa vya kujikinga na COVID - 19.
Wawezeshaji Vikundi vya Mabinti wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa vifaa vya kujikinga na COVID - 19.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Rafiki SDO limetoa msaada wa Vifaa vya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona 'COVID -19' kwa Wawezeshaji wa Vikundi vya Mabinti ngazi ya kata katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga.

Akikabidhi vifaa hivyo zikiwemo ndoo za kunawia mikono na sabuni leo Ijumaa Mei 29,2020 Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka shirika la Rafiki SDO, Dkt. Juma Jilala amesema vifaa hivyo vitawasaidia wawezeshaji hao kutoa elimu ya COVID -19 kwa makundi ya mabinti balehe ili wachukue tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona.

"Kupitia vifaa hivi watahamasisha mabinti waliopo katika maeneo yao kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ili kujikinga na maambukizi ya COVID -19",amesema Dkt. Jilala.

Kwa upande wake, Afisa Mwezeshaji Uchumi kwa Mabinti ngazi ya wilaya kutoka Shirika la Rafiki SDO, Asante Nselu alisema miongoni mwa majukumu ya Wawezeshaji wa Vikundi vya Mabinti ngazi ya kata  ni kutoa elimu ya uchumi,mabadiliko ya tabia kwa mabinti balehe walio nje ya shule,elimu ya malezi,ukatili wa kijinsia,ujasiriamali na masuala ya Ukimwi ili mabinti waweze kujitambua na kujikwamua kimaisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527