NDEGE ILIYOKUWA NA ABIRIA ZAIDI YA 100 YAANGUKA NCHINI PAKISTAN


Ndege ya Shirika la kimataifa la ndege la Pakistani -Pakistan International imeanguka katika mji wa Karachi ilipokuwa ikitoka Lahore, maafisa wa safari za anga wamesema.

Ndege hiyo Chapa PK8303, ambayo ilikuwa imewabeba abiria 91 na wahudumu wa ndege wanane, ilikuwa ikisafiri kutoka Lahore kuelekea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jinnah wenye shughuli nyingi zaidi nchini Pakistan.

Waziri wa afya wa jimbo amethibitisha vifo vya watu 11, lakini inahofiwa kuwa idadi ya vifo itaongezeka na kuwa ya juu zaidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527