NCHI 11 ZA ULAYA ZAAMUA KUFUNGUA TENA MIPAKA


Taarifa ya pamoja iliyotolewa na tovuti ya kidiplomaisa ya Ureno imesema, mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 11 za Ulaya wamekubali masharti ya kufungua tena mipaka na kurejesha uhuru wa mawasiliano kati ya wakazi wa Ulaya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wawakilishi kutoka Ujerumani, Austria, Bulgaria, Cyprus, Croatia, Hispania, Ugiriki, Italia, Ureno na Slovenia walishiriki kwenye mkutano kuhusu kurejesha uhuru wa mawasiliano na mzunguko kati ya Umoja wa Ulaya uliofanyika kwa njia ya video.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Heiko Maas amesema, Ujerumani itaondoa tahadhari ya utalii ndani ya Umoja wa Ulaya kuanzia tarehe 15 Juni, ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kupokea idadi kubwa ya watalii wakati wa msimu wa joto. 


Lakini hatua kadhaa za zuio zitachukuliwa katika sekta hiyo kutokana na kuwa mlipuko wa COVID-19 bado haujamalizika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527