MKUU WA MKOA WA TANGA APIGA MARUFUKU MAGARI YA MIZIGO YA KENYA KUINGIA NCHINI TANZANIA


Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ameziagiza mamlaka zote zilizopo katika mpaka wa Horohoro mkoani Tanga kutoruhusu gari lolote kuingia nchini kutoka nchini Kenya.

Shigella ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea eneo hilo na kukuta baadhi ya madereva wa Kitanzania wakiwa katika eneo hilo kwa zaidi ya siku sita bila ya kuruhusiwa kuingia upande wa Kenya.

Amesema kwa magari yoyote yanayotoka nchi za Rwanda na Burundi yaruhusiwe kupita katika mpaka huo wa Horohoro kwa kufuata taratibu zilizopo.

Aidha ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mpaka huo ili kuzuia watu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post