MABASI YA MWENDOKASI YAAGIZWA KUREJESHA HUDUMA YA USAFIRI KAMA KAWAIDA KABLA YA JUNE 01 | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, May 27, 2020

MABASI YA MWENDOKASI YAAGIZWA KUREJESHA HUDUMA YA USAFIRI KAMA KAWAIDA KABLA YA JUNE 01

  Malunde       Wednesday, May 27, 2020

Waziri wa Nchi , ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza wakala wa mabasi yaendayo haraka UDART kuhakikisha usafiri wa mabasi hayo unarejea kama kawaida kabla ya Juni Mosi, mwaka huu na kuondoa kero ya sasa inayowakumba abiria wanaotumia usafiri huo.

Selemani Jafo amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na msongamano mkubwa wa abiria kwenye vituo vya mabasi hayo kutokana na watu wengi kuanza kurejea kwenye shughuli zao mbalimbali kufuatia kupungua kwa ugonjwa wa corona.

“Ni kweli, baada ya Rais wetu, Dk John Pombe Magufuli kueleza matumaini makubwa ya idadi ya maambukizi kupungua nchini, watu wamerejea kwa kasi katika shughuli za kiuchumi, hii imechangia msongamano pale Kimara nyakati za asubuhi hasa tukikumbuka pia kuwa ni ‘level seat’,” amesema Jafo akizungumza na gazeti la Habarileo.

Jafo amesema kuwa wasimamizi wa mradi huo wamemueleza kuwa mbali na idadi ya watu kuongezeka, lakini idadi ya magari yanayotoa hudumu nayo imepungua, kwani mabasi marefu 30 yapo katika matengenezo.

Aidha, ameagiza magari hayo kufanyiwa matengenezo haraka, kwani kutokana na maisha kuanza kurudi katika hali kawaida, na vyuo kufunguliwa, usafiri huo utahitajika sana kuhakikisha watu wanawahi kwenye shughuli zao.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post