Korea Kusini Yaamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuuza vileo na kumbi za starehe baada ya kuzuka visa vipya vya Corona

Mamlaka za mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul zimeamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuuza vileo na kumbi za starehe baada ya kuzuka visa vipya vya virusi vya corona vinavyoibua wasiwasi wa kutokea wimbi la pili la kusambaa virusi hivyo hatari. 

Meya wa mji huo Park Won-soon amesema amri hiyo itakayoendelea bila kikomo imefuatia maambukizi mapya ya virusi vya corona yaliyogundulika kwenye wilaya ya Itaewon, yenye shughuli nyingi nyakati za usiku. 

Zaidi ya visa 24 vinahusishwa na mwanaume mmoja aliyegundulika kuwa maambukizi ya COVID-19 baada ya kutembelea kumbi tano za starehe kwenye wilaya ya Itaewon wiki iliyopita. 

-DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments