MWENDESHA BAISKELI MAARUFU 'DALADALA' AKUTWA AMEFARIKI DUNIA SHINYANGA MJINI


Mwendesha Baiskeli Maarufu ‘Daladala’ aliyejulikana kwa jina la Wakaka Kusaba anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32 hadi 35 amekutwa amefariki dunia ndani ya chumba alichokuwa anaishi katika Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio,mwendesha daladala huyo amekutwa amefariki dunia leo Jumanne Mei 26,2020 Majira ya saa moja usiku.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi, Bakari Hamis amesema mara baada ya kupata taarifa za kifo cha kijana huyo alitoa taarifa kwa Jeshi la polisi ambapo askari polisi wamefika eneo la tukio wakiwa na Daktari kisha kuuchukua mwili wa marehemu.

“Marehemu amejulikana kwa jina la Wakaka Kusaba alikuwa anafanya shughuli ya kubeba abiria kwa baiskeli hapa Mjini Shinyanga. Kwao ni Giliku wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu”,amesema Mwenyekiti wa mtaa.

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo,wamesema jana Makaka alikuwa mzima ingawa alikuwa analalamika kifua kinamuuma kutokana na kubeba gunia la mchele na muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na kikohozi na kwamba ndani ya chumba hicho kumekutwa damu zinazodaiwa kutapikwa na marehemu.

"Leo asubuhi pia alikuwa anasema anajisikia anaumwa, inawezekana amefariki dunia leo mchana",wamesema.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hili tutawaletea 
Askari polisi wakiwasili katika chumba ambacho Mwendesha baiskeli 'Daladala' Wakaka amekutwa amefariki dunia. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Askari polisi wakiongozwa na mwenyekiti wa mtaa wa Mabambasi Bakari Hamis (aliyevaa kofia) wakiingia katika chumba ambacho Mwendesha baiskeli 'Daladala' Wakaka amekutwa amefariki dunia
Askari polisi na daktari wakiongozwa na mwenyekiti wa mtaa wa Mabambasi Bakari Hamis (aliyevaa kofia) wakiingia katika chumba ambacho Mwendesha baiskeli 'Daladala' Wakaka amekutwa amefariki dunia.

 Mwili wa Mwendesha baiskeli 'Daladala' Wakaka ukitolewa ndani ya chumba alichokuwa analala.
Askari polisi wakiondoka na mwili wa marehemu Wakaka.
Wakazi wa Mabambasi wakiwa eneo la tukio.
Wakazi wa Mabambasi wakiwa eneo la tukio.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post