JOE BIDEN AMBAYE NI MPINZANI WA TRUMP UCHAGUZI WA MWAKA HUU MAREKANI AKANUSHA MADAI YA KUMDHALILISHA KINGONO MSAIDIZI WAKE


Mgombea urais nchini Marekani katika tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden, amekanusha vikali madai ya kumdhalilisha kingono Tara Reade ambaye alikuwa afisa wake wa zamani, huku akiongeza kuwa kisa hicho ambacho mwathiriwa anadai kilitendeka mwaka 1993, hakikutokea.
 

Akihojiwa na kituo cha televisheni cha MSNBC, Biden amekivunja kimya chake cha mwezi mmoja kuhusu suala hilo kwa kusema kuwa hajawahi kutenda uhalifu huo.

 Aidha, taarifa ya Biden imesema waliokuwa wasaidizi wake wakuu mnamo wakati kisa hicho kinadaiwa kutokea, wamekanusha kufahamu tukio hilo.

 Mgombea huyo wa Democrat amesema ataiomba idara ya taifa inayohusika na kuweka rekodi kuchunguza ikiwa kuna rekodi yoyote ya malalamiko hayo. 

Reade ni miongoni mwa wanawake ambao wamelalamika kwamba Biden aliwabusu na kuwashika kwa njia isiyofaa. 

Joe Biden atakiwakilisha chama cha Demokratic katika mchuano wa Urais  nchini Marekani Novemba Mwaka huu ambapo atachuana na Rais wa sasa  Rais Donald Trump


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post