RAIS UTPC : WAAJIRI KATIKA VYOMBO VYA HABARI WABORESHE MASLAHI YA WAANDISHI WA HABARI KIPINDI HIKI CHA COVID - 19

Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo

Leo ni Mei Mosi 2020, tukiadhimisha katika kipindi ambacho tupo katika vita kubwa ya kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.

Sekta ya Habari nchini Tanzania ni moja kati ya sekta ambazo zimeathiriwa sana na hali hii.

Wito wangu ni kwa waajiri yaani vyombo vya habari kuboresha maslahi ya waandishi wa habari kutoa ajira rasmi na kuwapa mikataba, kuthamini mchango wa waandishi wa haabri katika vyombo vyao, kulipa kwa wakati madai mbalimbali,kuanza kuwalipa waandishi walau kila wiki ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha kwa sasa kutokana na kutokuwepo kwa shughuli na baadhi yao kulazimika kukaa nyumbani.

Ni matumaini yangu wakati tukiadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi, waandishi wa habari nchini wanatumia siku hii kutafakari namna ya kuboresha kazi zao, kuongeza juhudi na maarifa, kuzingatia sheria na taratibu za nchi huku waajiri na wamiliki wakitafakari pia kuzingatia sheria za kazi na sheria nyingine ili kumfanya mwandishi na chombo cha habari kutenda haki na kuwajibika kwa umma.

Nawatakia Sikukuu Njema, TUFANYE KAZI KWA UANGALIFU, TUFUATE MAELEKEZO YA WATAALAMU, CORONA NI HATARI, IPO NA INAUA, TUJILINDE NA TUWALINDE WAPENDWA WETU.
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post