CHADEMA YAWAFUTA UANACHAMA WABUNGE WANNE

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetanganza kuwafuta uanachama wabunge wake wanne,Anthony Komu, Joseph Selasini,David Silinde na Wilfred Lwakatare.

Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ametangaza uamuzi huo leo yakiwa ni matokeo ya kikao cha Kamati Kuu ya chama.

“Kamati Kuu CHADEMA imeazimia Wabunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wameendelea kutoka kauli za kejeli, kashfa na kukiuka maagizo ya Chama, hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama” -John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA.

“Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama”- Mnyika

“Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA,  Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, ilitakiwa awe mfano na kwa kuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo”-Mnyika

“Kuhusu Wabunge wengine ambao wamekwena kinyume na maagizo ya Chama lakini hawajaonesha utovu wa nidhamu kwa kutoa kashfa kwa Chama, watatakiwa wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo” -Mnyika

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527