
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Dkt. Faustine Ndugulile (Mbunge wa Kigamboni) na kumteua Dkt. Godwin Oloyce Mollel (Mbunge wa Siha) kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
