ARUMERU WAZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA BARAKOA

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amezindua kiwanda kidogo cha kutengeneza Barakoa (mask) ikiwa ni sehemu ya jitihada za wilaya katika kupambana ma ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid - 19). 


Dc Muro ameweka wazi kuwa kiwanda hicho ni mali ya serikali ya wilaya kupitia Halmashauri ya Meru na kitakuwa na kazi ya awali ya kuzalisha Barakoa kwa ajili ya watumishi walio kwenye sekta ya afya ambao wako mstari wa mbele katika kupambana, na kusisitiza kuwa barakoa hizo sio za vitambaa vya kawaida bali zinatengenezwa kwa malighafi ambazo zinaviwango vya kukidhi na kudhibiti kusambaa kwa virusi kutokana na kutoruhusu hata maji kuingia kwenye barakoa hizo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post