MBUNGE AZZA HILAL AMWAGA VITABU NA MASINKI YA VYOO SHULE ZA WILAYA YA SHINYANGA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, May 8, 2020

MBUNGE AZZA HILAL AMWAGA VITABU NA MASINKI YA VYOO SHULE ZA WILAYA YA SHINYANGA

  Malunde       Friday, May 8, 2020
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa masinki ya vyoo 100 na maboksi 20 ya vitabu vya Masomo ya Sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Shinyanga vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5 ili kuboresha elimu katika wilaya hiyo.

Mbunge huyo amekabidhi vitabu na masinki hayo leo Ijumaa Mei 8,2020 wakati akikabidhi vitu mbalimbali ikiwemo gari la wagonjwa katika kituo cha afya Tinde,Ngao za uso kujikinga na COVID 19 kwa watumishi wa afya na kukabidhi bima za afya kwa wazee 17 waliopo katika kituo cha Usanda.

“Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko shule zetu zinakabiliwa na uhaba wa vyoo. Nimejaliwa kupata masinki 100 ya vyoo ili yakatumike katika ujenzi wa vyoo kwenye shule zetu zilizopo kwenye kata 22 zenye uhitaji wa vyoo”,alisema Mhe. Azza.

“Lakini pia nimeleta vitabu maboksi 20 kwa ajili ya shule za msingi na sekondari ambapo nimeleta maboksi 10 yenye vitabu vya masomo ya Sayansi kwa shule za sekondari na vitabu vya hadithi kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na vyenyewe maboksi 10”, alieleza Mbunge Azza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko aliwaagiza maafisa elimu kuhakikisha wanagawa vitabu hivyo kwenye shule zote pindi shule zitakapofunguliwa.

Mboneko alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi kuwalinda watoto wakati wa mapumziko ya Corona ikiwa ni pamoja na kutowaozesha watoto na kwamba hatapenda kuona wanafunzi wakiwa na ujauzito pindi shule zitakapofunguliwa.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko vitabu vya Masomo ya Sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa shule za  Sekondari katika wilaya ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 8,2020 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko vitabu vya Hadithi kwa ajili ya wanafunzi wa shule za  Msingi katika wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akisoma vitabu vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko moja kati ya masinki 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule mbalimbali kwenye wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba moja kati ya masinki 100 yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule mbalimbali kwenye wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post