WHO YAKANUSHA MADAI YA TRUMP KWAMBA INAIPENDELEA CHINA KUHUSU CORONA


Maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO wamekanusha leo kuwa shirika hilo linaipendelea China na kusema kuwa hatua hii hatari ya janga la virusi vya corona sio wakati wa kupunguza ufadhili, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa atasitisha ufadhili wake.

 Marekani ni mfadhili mkubwa wa shirika hilo lenye makao yake mjini Geneva ambalo Trump amesema lilitoa ushauri mbaya wakati wa mlipuko wa virusi vya corona. 

Mshauri mwandamizi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dr. Bruce Aylward, ameutetea uhusiano wa WHO na China, akisema kazi yake na mamlaka za China ni muhimu katika kuuelewa mlipuko huo ulioanzia mjini Wuhan. 

Naye Mkurugenzi wa kikanda wa WHO barani Ulaya Dr. Hans Kluge ameuelezea mlipuko wa virusi vya corona barani Ulaya kuwa wa wasiwasi mkubwa na akazitaka serikali kutafakari vya kutosha kabla ya kulegeza hatua za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post