WENYE VIRUSI VYA CORONA NCHINI KENYA WAFIKA 363


Waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe ametangaza kwamba watu 8 zaidi wamethibitishwa kuambikizwa virusi vya corona. Idadi ya Walioambukizwa Virusi hivyo nchini humo sasa imefika 363.


Wanne kati ya hao 8 wanatokea Mombasa huku waliosalia wakiwa ni wakazi wa Nairobi

Aidha, watu 8 pia wamethibitishwa kupona na kufikisha jumla ya idadi hiyo kufikia 114.

Wote walioambukizwa hawana historia ya kusafiri  nje ya nchi ikiwa ni sawa na kusema kwamba maambukizi hayo sasa ni ya ndani kwa ndani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post