WAZIRI MKUU UINGEREZA AENDELEA KUWA ICU KWA SIKU YA PILI SASA KWA CORONA


Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ametumia siku ya pili akiwa chumba cha uangalizi maalum wa matibabu (ICU) akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Covid-19.

Boris ambaye alibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona Machi 27 alipelekwa katika hospitali ya St Thomas Aprili 5 kwa vipimo zaidi baada ya hali yake kubadilika na Aprili 6 akapelekwa ICU.

Kwa mujibu wa Shirikia la Utangazaji Uingereza (BBC) limeripoti Waziri wa Afya, Edward Argar amesema hali ya Boris inaendelea vizuri.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Dominic Raab ambaye pia ana kaimu nafasi ya Boris amesema amekuwa akijiamini huku akimuita ni mpambanaji.

Raab amesema Boris amepatiwa matibabu ya hewa ya oxygen na akawa anapumua bila msaada wowote kama vile mashine ya upumuaji.

Raab amehakikisha kuwa Waziri Mkuu amekuwa akipata uangalizi mzuri wa kitabibu hospitalini hapo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post