WAGONJWA WA CORONA NCHINI KENYA WAONGEZEKA NA KUFIKA 225, MMOJA KAFARIKI LEO


Watu tisa zaidi wameambukizwa Virusi hatari vya Corona  Nchini Kenya  chini ya saa 24 zilizopita na hivyo kufanya idadi ya waliombukizwa virusi hivyo sasa kufika 225. 

Saba kati yao ni wakenya, wengine ni raia toka mataifa mengine

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe, leo Jumatano Aprili 15, amesema mtu mmoja pia amefariki kutokana na virusi vya ugonjwa huo  na kufanya idadi ya waliofariki kufika 10.

Amesema wagonjwa wengine  12   wamepona na hivyo kufanya idadi ya waliopona hadi sasa kufika 53


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post