UFARANSA YATAKA NCHI ZA AFRIKA ZISAMEHEWE MADENI YAKE YOTE ILI ZIWEZE KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA

Ufaransa na Ulaya wanatarajia kusaidia Afrika kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 kwa "kuifutia kabisa madeni yake," Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema Jumatatu katika hotuba kwa taifa. 


Rais Macron ameungana na baadhi ya viongozi duniani kutoa wito huo.

Jumatatu jioni, Emmanuel Macron amesikika akiunga mkono ombi lililotolewa hivi karibuni na viongozi kadhaa wa Afrika, ikiwa ni pamoja  kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis siku ya Jumapili.

Wito huo unakuja baada ya taasisi kadhaa za fedha za kimataifa kama vile IMF na Benki ya Dunia kutoa wito kwa nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda kusamehe madani kwa nchi za Afrika katika kuzisaidia kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. 

Ugonjwa huu ambao Umoja wa Mataifa uliutaja kuwa ni janga la kimataifa umeendelea kuwa tishio kubwa ulimwenguni hasa barani Afrika, ambapo nchini nyingi ni masikini, huku raia wao wakiishi katika mazingira magumu.

Suala hilo linatarajiwa kujadiliwa wiki hii na nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda, G20, kando ya mkutano wa Shirika la Fedha la Kimataifa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post