TRUMP AWATAKA WAMAREKANI KUJIANDAA KWA IDADI YA KUTISHA SANA YA VIFO VYA CORONA


Rais wa Marekani Donald Trump amewaonya Wamarekani kujiandaa kwa idadi ya kutisha sana ya vifo kutokana na virusi vya corona katika siku chache zijazo. 


Trump amesema Marekani inaingia katika kipindi ambacho idadi ya vifo itapanda kwa kasi. 

Hata hivyo, Rais huyo amesema Marekani haiwezi kuendelea kusitisha shughuli zake milele akiongeza kuwa itafika wakati ambao maamuzi magumu yatafanywa.

 Wakati visa vya maambukizi ya COVID-19 nchini Marekani vikithibitishwa kupindukia 300,000 kukiwa na zaidi ya vifo 8,300, kuna habari za kutia moyo nchini Italia na Uhispania ambako idadi ya imeanza kupungua. 

Sasa kuna visa milioni 1.17 vya maambukizi vilivyothibitishwa kote duniani na kumekuwa na vifo 63, 437 tangu mlipuko wa virusi hivyo ulipoanza nchini China mwaka jana. 

DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527