MTOTO WA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE AZIKWA, MAMIA WAMSINDIKIZA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 1, 2020

MTOTO WA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE AZIKWA, MAMIA WAMSINDIKIZA

  Malunde       Wednesday, April 1, 2020
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo ameongoza watumishi wa Ofisi yake katika mazishi ya Alazaro Sokoine ambaye ni mtoto Mkubwa wa Hayati Edward Moringe Sokoine. Mazishi hayo yamefanyika jana Monduli Juu Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu, jamaa na Marafiki.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akiweka shada la maua pamoja wanafamilia katika kaburi la kaka yake mkubwa Alazaro Sokoine. Mazishi yamefanyika jana Monduli Mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Bi. Emma Lyimo akitoa heshima za mwisho katika ibaada ya kuaga mwili wa Alazaro Sokoine ambae ni mtoto mkubwa wa Hayati Edward Moringe Sokoine. Mazishi yamefanyika jana Monduli Mkoani Arusha.
Wakuu wa Mikoa ya Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka, Morogogo – Mhe. Loata Sanare, Tanga – Mhe. Martine Shigela na Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakiweka shada la maua katika kaburi la Alazaro Sokoine, Monduli Mkoani Arusha.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post