DC SOPHIA MJEMA AAGIZA WANYWAJI POMBE WANUNUE WAKANYWEE NYUMBANI BADALA YA BAA


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amepiga marufuku mikusanyiko kwenye baa zote wilayani humo kuanzia jana  Ijumaa Aprili 17 ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona. 


Amewataka waendesha baa hizo, kuhakikisha wanauza vinywaji hivyo lakini lakini mnunuzi akanywee nyumbani na kwamba atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua.

“Ni wajibu wa kila mmoja kuzingatia maelekezo haya kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mwendeshaji wa baa na mtu yeyote atakayeonekana kwenye eneo la baa akiendelea kunywa,” amesema Mjema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527