MIKOA YA KANDA YA ZIWA YAKUBWA NA TETEMEKO LA ARDHI


Tetemeko la ardhi limetokea katika  Ukanda wa Ziwa Victoria na kuyakumba maeneo ya mikoa ambayo ni jirani na  Ziwa hilo  ikiwemo eneo la mpaka wa  Geita na Shinyanga.

Mjolojia Mwandamizi kutoka taasisi ya Jiolojia Bwana Gabriel Mbogoni amesema Tetemeko hilo lina ukubwa wa 4.6 katika Vipimo vya Richta.

Bwana Mbogoni amesema Tanzania imepitiwa na mkondo wa bonde la ufa la Afrika Mashariki ikiwa na mikondo miwili mkondo wa Mashariki na mkondo wa Magharibi hivyo matukio ya  mateteko ya ardhi kwenye mkondo wa bonde la ufa ni  lazima yotokee na kuwataka watanzania muda wote wawe kwenye hali ya tahadhari.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa tetemeko katika mkoa wake ambaye amesema Tetemeko hilo limepiga hadi Chato lakini hata hivyo haijasaabisha Madhara.

Mkoani Shinyanga hasa katika Wilaya ya Kahama ambayo inapakana na mkoa wa Geita kupitia kwa Mkuu wa  wilaya hiyo Bw. Anna Mringi Macha amethibitisha kutokea kwatuki hilo huku akieleza kuwa pia halijaleta madhara.

Credit:ITV


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527