MAREKANI YASEMA HUENDA WATU 240,000 WAKAFARIKI KWA CORONA NCHINI HUMO | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 1, 2020

MAREKANI YASEMA HUENDA WATU 240,000 WAKAFARIKI KWA CORONA NCHINI HUMO

  Malunde       Wednesday, April 1, 2020

Rais Donald Trump wa Marekani jana amesema nchi hiyo inakumbwa na changamoto kubwa zaidi kihistoria, na wiki mbili zijazo zitakuwa kipindi kigumu zaidi kwa nchi yake, na kusisitiza kuwa kufuata pendekezo la kujikinga na virusi vya Corona kunahusiana na uhai wa watu.

Mtaratibu wa Ikulu ya Marekani anayeshughulikia mambo ya kupambana na virusi vya Corona Bibi Deborah Birx amewaambia wanahabari kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya hali ya virusi vya Corona nchini humo. 

Makadirio yaliyotolewa naye yanaonyesha kuwa idadi ya vifo vya watu kutokana na virusi hivyo inaweza kufikia 100,000 hadi 2,40,000 chini ya hatua za udhibiti, na idadi hiyo ingefikia milioni 1.5 hadi milioni 2.2 bila ya kuchukua hatua hizo.

Ripoti iliyotolewa na Chuo cha udaktari katika Chuo Kikuu cha Washington imetabiri kuwa, hali mbaya zaidi ya kuenea kwa virusi vya Corona itatokea katika mwezi huu nchini humo, na itaendelea hadi mwezi Juni, na huenda ikatokea tena katika majira ya mpukutiko na majira ya baridi mwaka huu.

Kufikia sasa, janga la corona limesababisha zaidi ya vifo 3500 nchini humo na maambukizi ya zaidi ya watu 170,000.

Source:DW, CRI


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post