MABALOZI WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE CHINA KUZUNGUMZIA UBAGUZI WANAOFANYIWA WAAFRIKA CHINA


Mabalozi wa Nchi za Afrika wamekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje China, Chen Xiaoding kuzungumzia changamoto zinazowakabili baadhi ya raia wa Afrika katika mji wa Guangzhou.Chen amewaeleaza Mabalozi kwamba Serikali ya China haiungi mkono vitendo vya ubaguzi dhidi ya yeyote.

Kuhusu changamoto zilizowasilishwa na Mabalozi wa Nchi za Afrika zinazowakabili Waafrika nchini China, China imesema Mamlaka ya Jimbo la Guangdong itachukua hatua kuzishughulikia ikiwemo Raia wa Afrika ambao wameondolewa kwenye makazi na hoteli kupatiwa makazi mbadala ya muda.

China imewaahidi Mabalozi wa Nchi za Afrika kuwa itahakikisha zoezi la udhibiti wa corona linaendeshwa kwa usawa, kutoa elimu kwa umma ili kuepuka hatua zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni ubaguzi na Kuanzisha mtandao wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Nchi hiyo na Ofisi za Kibalozi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post