BIBI ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUBAKWA NA VIJANA AKITOKA KUTAFUTA TUMBAKU


Na Anthony Mayunga, Mwananchi 

Polisi wilayani Serengeti mkoa wa Mara wamemkamata mtuhumiwa mmoja kati ya wawili wanaodaiwa kumbaka mama mmoja mwenye umri wa miaka 58, mkazi wa Miseke ambaye amelazwa hospitali Teule ya Nyerere kwa ajili ya matibabu.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 6,2020 usiku katika kitongoji cha Senta wakati mama huyo (jina limehifadhiwa), mkazi wa kitongoji cha Majengo akitoka kutafuta tumbaku na mboga na inadaiwa watuhumiwa walimfuatilia kwa nyuma na kumkaba na kumfanyia ukatili huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah aliliambia Mwananchi kwa njia ya simu jana kuwa mtuhumiwa Kumari Mongita (23) mkazi wa kijiji cha Miseke amekamatwa na mmoja wanaendelea kumtafuta kwa kuwa alikimbia.

“Watuhumiwa walitajwa na mama huyo aliyefanyiwa ukatili na vijana hao, huyo mmoja kwa ushirikiano na wananchi tunaamini atakamatwa ili wafikishwe mahakamani baada ya taratibu kukamilika,” alisema .

Mganga mkuu wa hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba alidai mama huyo ana maumivu kifuani na sehemu nyingine za mwili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post