Picha : KASHWASA YATOA MSAADA WA MAPIPA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO DHIDI YA CORONA WILAYA YA SHINYANGAMkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mapipa 20 yenye ujazo wa lita 210 kila moja kwa ajili ya kukabiliana Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) inavyozalisha na kusambaza maji nchini imetoa msaada wa mapipa 20 yenye ujazo wa lita 210 kila moja kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga.Mapipa hayo yamekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko leo Alhamis Aprili 30,2020.

Mhandisi Mgeyekwa amesema KASHWASA itaendelea kushirikiana na serikaliH katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona kwani Corona inaweza kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi.

“Tumekabidhi mapipa 20 yenye ujazo wa lita 210 kila moja jumla lita 4,200 ambayo yatawekwa kwenye maeneo ya watu wengi katika wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona”,amesema Mhandisi Mgeyekwa

“Katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye mapambano dhidi ya Corona, KASHWASA imechangia mapipa 140 yenye thamani ya shilingi Milioni 11.8 kwa ajili ya wilaya 8 za mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Tabora ambako KASHWASA inafanya kazi zake ambapo kati ya mapipa hayo 140, 20 ni kwa ajili ya wilaya ya Shinyanga”,ameeleza Mhandisi Mgeyekwa.

Akipokea Mapipa hayo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameishukuru KASHWASA kwa mchango huo akibainisha kwa utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.

“Kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Shinyanga ninawashukuru sana  KASHWASA kwa kutupatia mapipa haya. Tutayapeleka katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili yakatumike kwenye maeneo ambayo yana mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo minada na masoko”,amesema Mhe. Mboneko.

“Mkurugenzi wa halmashauri na watendaji wengine hakikisheni mapipa/madumu haya yanakuwa masafi na yawe na maji muda. Simamieni pia wananchi wasiweke ndoo tupu bila maji na wanawe kwa maji na sabuni muda wote”,ameongeza Mboneko.

Aidha amesema serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu Corona kwa njia mbalimbali huku akiwasisitiza wazazi na walezi kuzuia watoto wasizurure mtaani watulie nyumbani na wafanyabiashara wasipandishe bei ya vifaa vinavyotumika katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba ameahidi kutunza mapipa hayo na kwamba yatawekwa kwenye maeneo yenye huduma za kijamii ikiwemo minada,masoko,zahanati na vituo vya afya.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) inavyozalisha na kusambaza maji katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, Mhandisi Joshua Mgeyekwa akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mapipa 20 yenye ujazo wa lita 210 kila moja kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga leo Alhamis Aprili 30,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akijaribu kufungua koki ya moja ya mapipa 20 yenye ujazo lita 210 kila moja yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kupokea mchango wa mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiishukuru KASHWASA kwa mchango wa mapipa 20 kwa ajili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga ambapo alisema mapipa hayo yatapelekwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority (KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) mapipa 20 kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) mapipa 20 kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba (kulia) mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA ili yakatumike kwenye maeneo yenye huduma za kijamii katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akizungumza baada ya kupokea mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA ili yakatumike kwenye maeneo yenye huduma za kijamii katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Muonekano wa mapipa yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya mapambano dhidi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (kushoto) akimpa zawadi ya Kalenda za KASHWASA Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko baada ya kukabidhi mapipa 20 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (kulia) akimpa zawadi ya Kalenda za KASHWASA Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba baada ya kukabidhi mapipa 20 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post