JIJI LA DODOMA LABADILISHA MFUMO WA UUZAJI MAENEO TAHADHARI YA CORONA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Kufuatia tishio la kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona,Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amelazimika kubadilisha mfumo wa uuzaji fomu kwa ajili ya maeneo kutoka njia ya kawaida na kuanzisha mfumo wa kidijitali.

Akizungumza na waandishi wa habari  April 8,2020jijini Dodoma Mkurugenzi  wa jijni hapa Godwin Kunambi amesema uuzwaji wa fomu hizo kwa njia ya mtandao utawapa fursa wale wote ambao hawapo Dodoma kujaza fomu hizo wakiwa kwenye maeneo yao badala ya kufunga safari hadi Dodoma.

Kuhusu wananchi waliokuwa tayari wamekwisha lipia na kuchukua fomu hizo KUNAMBI amesema wote wataingizwa kwenye mtandao ambapo pia mfumo huo utaanza kutumika rasmi April 14 mwaka huu.

Aidha  amesema muda wa uuzwaji wa fomu kwa njia ya mtandao utakuwa kwa muda wa siku saba na fomu moja itauzwa kwa gharama ya Sh20,000.

Awali zoezi hilo liliwalazimu wananchi kufika moja kwa moja katika Ofisi za iliyokuwa manispaa ya zamani lakini kutokana na mwitikio mkubwa imeonekana kukawepo uwezekano wa kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Corona hivyo kulazimika kusitishwa kwa zoezi hilo na badala yake kutangazwa kufanyika kwa njia ya mtandao


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527