JAMBO KARANTINI LIVE KUUNGURUMA JUMAMOSI HII APRILI 25,2020..... #STAYHOME CORONA IPO CHUKUA TAHADHARI....USIKOSE
Karibu katika Jambo Karantini Live Episode ya Kwanza Jumamosi hii Aprili 25,2020 kuanzia saa 2 kamili usiku hadi saa 5 usiku kwa ajili ya kufurahia muziki,kupata elimu kuhusu Corona, kuchemsha ubongo na kupata zawadi mbalimbali kupitia INSTA LIVE ukurasa wa Instagram wa JamboGroup.

Jambo Karantini Live inayoendeshwa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products inalenga kuhamasisha watu wakae ndani wasitoke kwenda sehemu ya nje kupata burudani ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona (Covid - 19).

Jumamosi hii kutakuwa na Ma DJ wawili (Dj Dhifa Untouchable na Dvj Nicky The Best) ambao watatoa burudani live kupitia JamboGroup pia Watangazaji Kenedy The Remedy na Saramike wakiwa na Mgeni wa Heshima 'VIP Guest' watatoa elimu kuhusu Corona, Chemsha Bongo na zawadi kwa watu watakao jibu maswali kwa usahihi kupitia Insta Live ya JamboGroup.

Burudani inarudi Kiganjani mwako, Andaa Kinywaji chako ufurahie zaidi.

Ili kupata Uhondo wote Tu - Follow Instagram JamboGroup

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post