WAGONJWA WAPYA 84 WA CORONA WAONGEZEKA TANZANIA,WANATOKA MIKOA MBALIMBALI IDADI YAFIKA 254



Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imethibitisha kuwepo kwa Wagonjwa wapya 84 wenye maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID -19) nchini Tanzania. Kati ya hao wagonjwa 16 ni waliotolewa taarifa na Waziri wa Afya wa Zanzibar leo Aprili 20,2020. 

Kwa upande wa Tanzania Bara Idadi ya wagojwa na mikoa wanayotoka  ni Dar es salaam (33), Arusha (4), Mbeya (3), Kilimanjaro (3), Pwani (3), Tanga (3), Manyara (2), Tabora (1),Dodoma (3), Ruvuma (2),Morogoro (2), Lindi (1), Mwanza (3),Mtwara (1), Kagera (1),Rukwa (2)



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527