BARAZA LA MAASKOFU -TEC LASITISHA UIMBAJI KWENYE IBADA ZA MISA ILI KUKABILIANA NA CORONA


Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ‘TEC’ limetoa tamko kutekeleza agizo alilotoa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Aprili 15, juu ya kujilinda na  Corona kwenye masuala ya ibada.


TEC imeamua kusitisha mazoezi ya kwaya ili kuepuka mikusanyiko. Pia nyimbo wakati wa ibada zimesitishwa ili Ibada isitumie muda mrefu

Pia mafundisho ya dini kwa watoto na makundi mengine yamesitishwa. Mafundisho yataendelea kwa njia nyingine kama kujisomea katekisimu au njia ya mtandao

Pia kanisa litazingatia umbali wa mtu na mtu wanapokuwa ibadani, matumizi ya vinasa sauti, watanawa mikono kabla ya kuingia kanisani pia watanyunyizia dawa vifaa vya ibada


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post