WATEJA WA TIGO PESA SASA WANAWEZA KUTUMA NA KUPOKEA PESA KUTOKA M-PESA YA KENYA, MTN NCHINI UGANDA, AIRTEL NA MTN NCHINI RWANDA


Dar es Salaam: 14 Aprili, 2020. Tigo Tanzania, kampuni inayoongoza kwa ubunifu wa Kidigitali nchini, leo imezindua huduma inayowawezesha watumiaji wote wa Tigo Pesa nchini Tanzania kuweza kutuma na kupokea pesa kupitia simu zao za mkononi kutoka M-PESA ya Kenya, MTN nchini Uganda, Airtel na MTN za nchini Rwanda.
Huduma hii ni wazi sasa kwamba inawaunganisha wateja wa Tigo Pesa na mitandao mingine mikubwa ya mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki inayotoa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi hatua ambayo itakuza wigo wa kufanya mihamala ya kifedha bila kujali mipaka baina ya nchi moja na nyingine.
Kaimu Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Tanzania, Angelica Pesha, amesema, “Huduma hii mpya baina ya nchi nne inadhihirisha namna Tigo ilivyojidhatiti kwenda sambamba na mahitaji ya wateja wake kwa kutuo majawabu ya kidigitali. Na pia hii maana yake faida za mihamala ya kifedha kupitia simu za mkononi itakuza biashara baina ya nchi hizi hivyo kuwezesha biashara pamoja na familia kutuma na kupokea pesa kwa uharaka na usalama zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ushirikiano huu unaifanya kampuni yetu kuwa chaguo la wengi katika masuala ya huduma za kifedha na tunaamini kwamba hatua hii mpya itaweza kukuza mihamala ya kifedha pamoja na biashara katika mataifa yote manne.”
“Kutuma pesa kwa watoa wateja wa watoa huduma wengine, wateja wa Tigo Pesa wanaweza kupiga *150*01# katika simu zao, kisha chagua tuma pesa, nje ya nchi, chagua kati ya Kenya, Uganda au Rwanda.” Pesha amefafanua.

ANGALIA HAPA MKUTANO KWA VYOMBO VYA HABARI ULIOFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO MTN Uganda imekuwa siku zote mstali wa mbele katika ubunifu na utoaji wa huduma za kifedha ikiwemo kuanzisha mikopo midogo midogo na mikubwa, bima, na njia ya malipo ya kielekitroniki iitwayo MoMoPay.

“Ili kuwezesha mtandao wetu wa huduma za kifedha kuwafikia wateja wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki, huu ni ushuhuda kwamba tunaendelea kufanya jitihada za kupanua huduma zetu nafuu, za uhakika na salama sio tu kwa wateja wetu wa nchini Uganda bali ni kwa watu wote wa ukanda huu,” amesema Stephen Mutana, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa MTN Uganda.
Wakati huduma za kifedha kupitia njia ya simu za mkononi ikiwa haina mipaka, ushirikiano huu mpya na Tigo Tanzania ni sehemu ya kujitoa kwetu kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wateja wetu ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hii inatoa fursa kwao kuweza kutuma na kupokea pesa kutoka au kwenda kwa marafiki, ndugu pamoja na wabia wa kibiashara kwa kutumia Airtel Money.
Wakati kupokea pesa kutoka Tigo Tanzania ni bure, kutuma pesa kwenda Tigo Tanzania, wateja wa Airtel Money wanapaswa kupiga *500*1*3# na kufuata malekezo,” amesema Jidia Gasana wa Airtel Rwanda.
Ushirikiano huu mpya baina ya Safaricom, MTN, Airtel na Tigo Tanzania unatuwezesha kufikia mahitaji ya kufanikisha mihamala ya kifedha ndani ya Afrika Mashariki. M-PESA imekuwa huduma inayokubalika na wakenya wengi kimataifa ambao wamekuwa wakiiona kuwa ya haraka, salama, yenye unafuu na rahisi.
Ili kutuma pesa kwa watoa huduma wengine, wateja wa M-PESA wanaweza kupiga *840# katika simu zao au kupitia mySafaricom App kwa kuchagua kipengele cha ‘M-PESA Global’ kilichokoo ndani ya M-PESA na kisha kuchagua ‘Tuma’

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post