WIZARA YA MAJI YAFUTA SHUGHULI YA WIKI YA MAJI 2020 KUWEKA TAHADHARI YA CORONA


Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa Ulimwengu Mzima ukikumbwa na Taharuki ya ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona ,Wizara ya Maji imefuta shughuli  zote kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi hivyo.

Katika taarifa iliyotolewa  leo Machi 16,2020  na kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maji ,kwa Umma  imefafanua kuwa shughuli zote zilizokuwa zifanyike kuelekea siku ya maji duniani.

Hivyo,Taarifa hiyo imefafanua kuwa hafla za uzinduzi wa miradi ya maji na mikutano yote ambayo ilikuwa ifanyike  katika wiki hii imefutwa  huku wizara ikiomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa wadau wote .

Ikumbukwe kuwa Mataifa mbalimbali yamejawa na hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo hapa Tanzania kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amethibitisha kuwepo kwa kisa cha mtu mmoja Mtanzania mwanamke  [46]ambaye aliwasili na ndege ya Rwandair  akitokea nchini Ubelgiji  na kushukia katika uwanja wa ndege wa KIA na alifikia katika hotel ya  Mt.Meru jijini Arusha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527