WATATU WAKAMATWA KWA KUUA NA KUFUKIA MWILI KATIKA SHAMBA LA MAHINDI

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

JESHI la Polisi mkoani Pwani, kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 51, raia wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini kupitia bandari bubu ya Makurunge katika wilaya  ya Bagamoyo.

Idadi hiyo inafikia wahamiaji haramu 100 baada ya wengine 49 kukamatwa juzi ,Kidomole,Fukayose.

Kamanda wa polisi mkoani hapa,Wankyo Nyigesa alieleza, raia hao wamekabidhiwa kwa vyombo vya dola kwa taratibu za kisheria .

“Raia hawa wamekamatwa usiku wa kuamkia march 20 huko Makurunge, kata ya Makurunge, Tarafa ya Yombo, Wilaya ya Bagamoyo”alifafanua Wankyo.

*AKAMATWA AKISAFIRISHA VIROBA VITANO VYA  BANGI*
Jeshi hilo, linamshikilia Ally Hashimu Athumani ,mkazi wa Malela – Morogoro kwa kosa la kusafirisha bangi viroba vitano. 

“Mnamo march 20 ,majira ya saa 12:00 huko maeneo ya Maili moja, Kata ya Maili moja,Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani Jeshi la Polisi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema  walimkamata mtuhumiwa huyo akisafirisha kiasi hicho cha bangi kutoka Morogoro kuelekea Dar Es  Salaam kwa kutumia gari yenye namba za usajili *T.688 CZK* ,Toyota Carina nyeupe”:.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

WATATU WAKAMATWA KWA KUUA NA KUFUKIA MWILI KATIKA SHAMBA LA MAHINDI
Mnamo tarehe 10/03/2020 majira ya saa 14:30 hrs huko maeneo ya  Kibindu, Kata ya Kibindu,Tarafa ya Chalinze katika Wilaya ya kipolisi Chalinze, Mkoa wa Pwani *Bw. Chacha Chacha Machangu,* Miaka 27,Mkurya, mkazi wa Kibindu alimfumania mke wake (jina linahifadhiwa ) akiwa na mwanaume mwingine na mara baada ya tukio hilo alimshambulia kwa kumkata kata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo cha mama huyo usiku wa tarehe 10/03/2020.

Baada ya tukio la kifo cha mama huyo Bw Chacha Machangu kwa kushirikiana na ndugu zake ambao ni *Emmanuel Chacha Machangu,* Miaka 19,Mkurya na *Hamis Chacha Machangu*, Miaka 22, Mkurya,wote wakazi wa Kibindu walichimba shimo katika shamba la mahindi na kuufukia mwili wa mama huyo.

Mnamo tarehe 19/03/2020 Jeshi la Polisi (M) Pwani lilipata taarifa ya tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote watatu waliojihusisha na tukio hilo na wao wenyewe kwa ridhaa yao walionesha mahali shimo lilipo.Baada ya Jeshi la Polisi kufukua ulipatikana mwili wa marehemu ambao ulifanyiwa uchunguzi na daktari kisha kufanyiwa mazishi kwa heshima zote.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527