UONGOZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAKUTANA NA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO KUJADILI FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO


Waziri wa  Maliasili  na  Utalii, Dkt.  Hamisi Kigwangalla, jana amekutana na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro, Viongozi wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro.

Fedha hizo sasa zitapelekwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro  kutekeleza shughuli zilezile zilizokuwa zinatekelezwa na Baraza la Wafugaji Ngorongoro.

Mkutano huo uliofanyika  kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Swagaswaga, umehudhuriwa na Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utaliii Mhe. Constantine  Kanyasu, Mbunge wa Ngorongoro  na Naibu Waziri wa Elimu,  Sayansi, na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda ,  Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Rashid Mfaume Taka na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Maurus Msuha.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Prof. Abiud Kaswamila, Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Freddy Manongi, Meneja wa Maendeleo  ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,  Bw. Fedes Mdala.  na Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro,  Bw. Edward Maura.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post