WANAWAKE TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA (TCDC) WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa
tayari kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Jijini
Dodoma
 Picha
ya Pamoja ya Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa tayari
kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Jijini Dodoma


Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa na Bango la
maandamano lenye Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
 Wanawake
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakibeba bango la maadhimisho mbele ya
meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, Jijini
Dodoma

=======  ========  ========

Wanawake wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika Jumapili 8 Machi, 2020 wameungana na wanawake
wengine Duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Jijini
Dodoma.

Wanawake hao wameadhimisha Sikukuu hiyo kwa shughuli
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushiriki maandamano yaliyofanyika katika
viwanja vya shule ya msingi Mkonze. Maandamano ambayo yalipokelewa rasmi
na Mgeni Rasmi Mhe.Felista Bura (Mb) Kata Mkonze, Jijini Dodoma.

Sherehe
hizo zilipambwa kwa Kauli mbiu isemayo “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo
ya Tanzania ya Sasa na baadae” pamoja ujumbe kutoka Tume ya Maendeleo ya
Ushirika usemao “Wanawake Tuamke na Fursa za Ushirika”

Siku hii
maalum huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kukumbuka na kutafakari juu
ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na
msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.

Veneranda
Mgoba Afisa Ushirika wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika katika mahojiano
na waandishi wakati wa maadhimisho hayo ametoa wito kwa wanawake
kushiriki fursa zilizopo katika vyama vya Ushirika nchini ili
kujiimarisha na hatimaye kuondokana na utegemezi pamoja na umaskini.
Akiongeza kuwa ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi bado ni
mdogo kulinganisha na wanaume. Hivyo, amewataka wanawake kushiriki na
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vya Ushirika.

“Wanawake
wenzangu tujiunge na Vyama vya Ushirika vya kifedha kama vile vyama vya
Akiba na Mikopo (SACCOS) pamoja na vile visivyo vya kifedha kama vile
AMCOS ili kuhakikisha tunapata fursa za kujiendeleza kiuchumi,” alisema
Veneranda

Wanawake wa Tume waliendelea na maadhimisho hayo kwa
kutoa msaada wa vifaa vya mahitaji mbalimbali kwa wanawake wenzao kwa
lengo la kuendeleza upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa wanawake na
jamii kwa ujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post