Rais Magufuli Atoa Billioni 15 Kumalizia Ujenzi Hospitali Ya Mwalimu Nyerere Mara


Na Mwandishi Wetu Musoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha shillingi Billioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyojengwa kwa miaka 40 bila kumalizika.

Haya yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika hospitali hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi wake.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Hospitali hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali hiyo itakuwa masaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara hasa kwa huduma za matibabu ya kibingwa.

“Kutakuwa hakuna haja ya kwenda Hospitali ya Kanda Bugando kupata matibabu ya kibingwa kwani tunataka huduma za kibingwa zitolewe hapa hapa”alisema

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Shirika la Nyumba na Chuo Kikuu cha Ardhi kimepewa kazi ya kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo hivyo ameagiza kazi kufanyika usiku na mchana ili limalizike kwa muda uliopangwa.

“Tumekubaliana tarehe 17 mwezi huu wa tatu wawe wamekamilisha Wing C ili huduma za Mama na mtoto zinanze kutolewa kwa muda husika” alisema

Kwa upande wake Mkuu Mkoa wa Mara Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia hospitali hiyo iliyokwama kwa muda wa miaka 40 mpaka sasa.

“Hospitali hii imechukua awamu tano za marais kumalizika na tunamshukuru Rais kwa kuchukulia kipaumbele katika hili” alisema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post