RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM.....ATANGAZA KUAHIRISHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2020


Rais  wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amesitisha  mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2020.
 
Mbio hizo zilitarajiwa kuanza hivi karibuni.Uamuzi huo ni tahadhari ya kuepukana na maambukizi ya CORONA.


Ugonjwa huo uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 6,513 katika nchi mbalimbali umeingia Afrika Mashariki katika nchi za Kenya, Rwanda.



Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la juu eneo la Ubungo linalounganisha barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela.



“Nina fahamu kitu kingine kinacholeta mkusanyiko ni mwenge na tulitegemea kuwasha mwenge karibuni kule Zanzibar ambapo ungewezwa kutembezwa nchi nzima, nimeamua mbio za mwenge hazitafanyika mpaka corona iwe imeondoka” amesema Magufuli.



Rais Magufuli amesema fedha za mwenge ambao ulitakiwa kuwashwa Zanzibar zitatumika katika kujiandaa na tahadhari zaidi ya corona ambayo ishafika Kenya na Rwanda.

Amesema hadi sasa hakuna mgonjwa wa corona Tanzania na mbio za mwenge zitaendelea  itakapothibitishwa ugonjwa huo umeisha duniani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527