Breaking : SOKO KUU MJINI SHINYANGA LANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO USIKU HUU

Soko Kuu Mjini Shinyanga limenusurika kuteketea kwa moto baada ya moto ambao haujajulikana chanzo chake kuunguza baadhi ya bidhaa ikiwemo maboksi na madumu na ndoo za plastiki.Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde 1 blog iliyofika eneo la tukio kuwa moto huo umeanza kuwaka leo Jumamosi Machi 21,2020 majira ya saa moja na nusu usiku.

“Tukiwa nje ya Soko Kuu tumesikia yowe la watu wakipiga kelel tukafikiri labda ni wezi, Baadaye tukasikia Moto! Moto! Moto!,ikatubidi tuwahi,tukaingia ndani ya soko na kuona moto eneo la choo unawake ukiunguza bidhaa mbalimbali,Wasamaria wema waliokuwepo tumeshirikiana kuzima moto huu kwa maji”,amesema mmoja wa wananchi aliyejulikana kwa jina la Suleiman Abeid.

“Lakini moto huu umetushangaza kwani umewaka katika mazingira ya kutatanisha.Hii hali lazima ichunguzwe kwanini moto huo umewaka.Kuna vifaa vya mfanyabiashara ambaye huuza maboksi,kuna ndoo na maboksi kadhaa zimeungua hapa”,ameeleza Abeid.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliojitokeza kuzima moto huo ambao umetokea wakati Umeme ukiwa umekatika Mjini Shinyanga,wamesema huenda moto huo huenda umetokana na sigara iliyorushwa na mtu aliyekuwa ndani ya choo ama moto huo umewekwa kwa maksudi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa katika soko hilo kuna mgogoro wa vyumba.

Wananchi hao wameziomba Mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo la moto.
Endelea kufuatilia habari zaidi kupitia Malunde 1 blog
Baadhi ya bidhaa zilizoungua katika Soko Kuu Mjini Shinyanga baada ya kutokea kwa moto ambao haujajulikana chanzo chake usiku huu Jumamosi Machi 21,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post